GuidePedia

0

WANANCHI wa Vijiji vya Ndoa,liunji,Kimata na Makaonde kata ya Makaonde Tarafa ya mwambao wilayani Ludewa mkoani Njombe wameulalamikia uongozi wa vijiji hivyo pamoja na kata kwa ujumla kwa kushindwa kusimamia na kutelekeleza shughuri za maendeleo ya kata hiyo kwa zaidi ya miaka nane.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika  walipotembelewa katika vijiji hivyo walisema kuwa wamekuwa wakijitahidi kuchangia nguvu kazi zao katika shughuri za maendeleo lakini serikali za vijiji hivyo imekuwa ikikwamisha shughuri za maendeleo kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi huku jitihada za ujenzi wa miradi ikisuasua.

Alfan Ngoye na Wilson Kaluwa kutoka kijiji cha Makonde walishusha tuhuma kwa Diwani wa kata ya Makaonde Chrispin Mwakasungura (MWENDAKOTE)pamoja Mwenyekiti wa kijiji hicho Sosten Haule(KISADO)kuwa ndiyo kikwazo cha maendeleo katika kata hiyo kwa kushindwa kusimamia miradi kadhaa iliyotengewa bajeti na Serikali.

Waliitaja miradi ambayo imetengewa bajeti na wao kushindwa kusimamia kuwa ni madaraja ambayo baadhi yamejengwa chini ya kiwango,ukarabati wa kituo cha afya ambacho kilitengewa fedha zaidi ya million 20 lakini kilichofanyika ni kupaka rangi tu na fedha hazijurikani zimetumika kiasi gani na kuwa vibarua waliokuwa wakisaidia ujenzi hawajapata stahiki zao.

Waliutaja mradi mungine kuwa ni ujenzi wa nyumba mbili za waalimu ambao haujakamilika wakati Serikali ilitoa pesa na wananchi kuchangia nguvu zao kwa kuchangia matofali lakini hawajui ni lini ujenzi huo utakamilika na kuwa kutokana na hali hiyo wamedai kuwa wamevunjwa moyo wa kuchangia nguvu kazi zao kwani zinapotea bure.

Walizitaja changamoto zilizopo kwenye vijiji hivyo kuwa ni tatizo la mawasiliano ambapo wengi wao utembea umbali mrefu kutafuta network ikiwemo ya kupanda juu ya miti ili simu ziweze kukamata,ukosefu wa barabara ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa mitumbwi na maboti kufuata huduma za kijamii kwenye soko,ukosefu wa wauguzi katika kituo cha afya waliopo wapo 3 wanaohudumia watu zaidi ya 6,000 ukosefu wa shule za kata ambapo katika 3 za mwambao huo hutegemea shule sekondari ya Makonde.

Katika hatua nyingine wananchi wa kata hiyo wameitaka serikali ya kata hiyo kuwaondoa wananchi wa kitongoji cha Mpasya waliojenga maeneo hatarishi ambao makazi yao yamezungukwa na visiwa kuwa iwapo hawatahama maeneo hayo maisha yao yapo hatarini pindi mvua za masika zitakapoanza kunyesha mfurulizo.

Frank Mapunda mkazi wa kitongoji hico alisema kuwa eneo hilo lipo bondeni na pia limezungukwa na visiwa vinavyotiririsha maji kutoka katika milima mirefu iliyopo nyuma ya nyumba hizo hivyo kama hawata tafuta maeneo mengine ya kujenga makazi mapya basi maisha yao yapo hatarini iwapo mvua za masika zitaendelea kunyesha.

Alisema serikali ya kijiji hicho pamaja na kata kwa ujumla iwapo hawatawahimiza wananchi hao kuyahama makazi hayo ambao wameonekana kuwa wazito kuyahama makazi hayo kwa madai kuwa hawana uwezo wa kujenga nyumba zingine ambapo baadhi yao walipohojiwa na gazeti hili walidai watahama pindi watakapo pata pesa.

Alipotafutwa Diwani wa yata hiyo ya Makonde Chrispin Mwakasungura ofisini kwake lakini hakupatikana na alipopigiwa simu ii kuyatolea ufafanuzi madai haya simu yake haikupatikana kutokana na tatizo la mtandao wa mawasiliano  linalovikabili vijiji vya Tarafa hiyo ya Mwambao vilivyopo pembezoni mwa ziwa nyasa.

                                                                           Na, Ibrahim Yassin

Post a Comment

 
Top