GuidePedia

0
JAMII imetakiwa kujitolea kujenga majengo ya mahakama sambamba na nyumba za kuishi mahakimu na watumishi wengine wa mahakama ili waweze kufanya kazi zao kwa amani na utulivu kitu kitakachowafanya wao kutenda haki

Wito huo umetolewa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo uambatana na dua za viongozi wa dini mbalimbali kama isharra ya kuanza kwa kazi za mahakama kwa mwaka huu wa 2014
Alisema kuwa ufike wakati jamii kama ndiyo wadau wakuu wa mahakama wakajenga utamaduni wa kuanza kujitolea kujenga majengo ya mahakama na nyumba za watumishi kama ambavyo wanavyofanya kwenye ujenzi wa zahanati,shule,nyumba za walimu na mambo mengine kwani hiyo ndiyo njia rahisi ya jamii kupata huduma za kimahakama karibu

Alisema kuwa kama wananchi wataonyesha moyo wa kujitolea kufanya kazi hiyo serikali haitawaacha bali ni lazima itaunga mkono jitihada za wananchi katika kufanikisha lengo lao la kuwa na mahakama nzuri nay a kisasa

Rugemalila alisema kuwa siku ya sheria kwa mwaka huu imebeba ujumbe kuwa utendaji haki kwa wakati,umuhimu wa ushiriki wa wadau ambapo alisema kuwa ujumbe huo umekuja kwa wakati hususani wilayani Nkasi kwani utendaji haki unategemea zaidi wadau wengine kama polisi,jamii yenyewe kutoa ushahidi na wengineo,hivyo kila mmoja anatakiwa kuwajibika
Pia alisema kuwa mahakama yake moja ya changamoto kubwa inayokumbana nayo ni kukosekana kwa gereza la mahabusu kitu kinachowapa shida polisi na kuwaingiza gharama na wakati mwingine watuhumiwa kushindwa kufika kwa wakati mahakamani kutokana na kukosekana kwa usafiri wa uhakika na kuwanyima haki wanayostahili kuipata kwa wakati

Wakiri wa kujitegemea kutoka chama cha wanasheria Tanganyika tawi la Rukwa na Katavi Ileth Mawala alisema kuwa wadau wana nafasi kubwa ya kuhakikisha kesi zinakwisha kwa wakati endapo kila mmoja atawajibika ipasavyo

Alisema kuwa haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa hivyo ipo haja kwa wadau wote wakiwemo mawakili kuhakikisha kuwa kesi zote nikwisha kwa wakati na kudai kuwa ozoefu unaonyesha kuwa kesi nyingi zilizo na mawakili uchukua muda mrefu na kuwataka sasa wawajibike na kuacha kuziairisha kesi kila wakati bila ya sababu za msingi,ambapo hata wakiri wa serikali mkoani Rukwa Fadhiri Mwandoloma naye alikazia hoja hiyo huku akisisitiza kuwa kucheleshwa kwa haki ni sawa kabisa na haki hiyo kuwa imekataliwa

Mkuu wa wilaya Nkasi Idd Hassan kimanta ambaye aliwakilishwa na katibu tawala wa wilaya Festo Chonya alisema kuwa haki inayopatikanika kwa wakati huondoa shaka kwa mahakama na kuwa hilo ni lazima lisimamiwe na kuwa serikali kama mdau mkubwa itahakikisha inafanya mchakato wa haraka wilayani Nkasi kunapatikanika gereza la mahabusu ili watu waweze kufika mahakamani kwa wakati

Na alimtaka kila mmoja kuitafuta haki yake mahakamani na kuwa kama akiona kuwa hajatendewa haki na vizuri kwenda mahakama ya juu zaidi ya ile ya awali na kuwa hiyo ndiyo njia pekee na siyo kukimbilia mahakamani pale anapoona ameonewa na mahakama

Post a Comment

 
Top