GuidePedia

0


Wafanyabiashara wa jijini Mbeya wameingia katika mgogoro wa kupinga mashine za kielectronic za kutolea risiti ikiwa leo ni siku ya pili, huku wakidai kuwa zinawapa hasara kubwa kwao na kupeleke akufunga maduka yao.
Wakionge na lumemo blog wafanyabishara hao walisema kuwa sababu inayo wafanya kupinga kutumia mashine hizo ni kwamba zinamakato makubwa katika biashara wanazozifanya.
Walisema kuwa mpaka leo ni siku ya tatu tangu wafunge maduka hayo, “sisitangutufungemadukayetuleonisikuyatatunatumeamuakufungamadukayetusisiwenyewewalasiyo TRA kwa sababu tumewaona wenzetu katika mikoa mbali mbali kama vile Dar es salaam na sehemu nyingine”
Adha walisema kutokana na kipato wanachokipata katika biashara hizo ni kidogo hivyo nivigumu kuweza  kumudu gharama z amashine hizo.
Hata hivyo Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya Anody Maim, amesema kufungwa kwa maduka na mashine za EFD ni vitu viwili tofauti hivyo anawashangaa  wafanyabishara hao kufunga maduka yao pasipo sababu ya msingi.
Aidha amesema kuwa moja kati ya sababu ya kufunga maduka yao wafanyabishara hao ni kutopata elimu ya kutosha kuhusu mashine hizo na kwamaba hawana tabia ya kuhudhuria semina zinazotolewa na TRA.
Kwani mara nyingi wamekuwa natabia ya kuwatuma wafanyakazi wao kufika katika semina elekezi zinazotolewa na TRA zinazohusu umuhimu wa kutumia mashine hizo.

Post a Comment

 
Top