GuidePedia

0

waliosimama mbele kushoto ni mkuu wa shule Eckson Mwakalikamo akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa vanessa, Bi, Shukran Gidion.
kulia mkuu wa shule ku;lia Mwakalikamo kushoto mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Vanessa Bi Shukran Gidion akihutubia katika ukumbi wa shule.
Moja kati ya walimu waliyotunukiwa zawadi siku hiyo.
Diwani wa kata ya Isyese Sanke Sesoakihutubia.
.................................................................................


Mkurugenzi wa TEHLAH FOUNDATION  Bi. Shukurani Gidion ambayo inamiliki shule ya sekondari ya Vanessa iliyopo Kata ya Isyesye Jijini Mbeya ametoa tuzo kwa Walimu na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kufanya vizuri mtihani wa kidato cha pili kimkoa na kitaifa.
Hafla ya kutunuku tuzo hizo imefanyika katika ukumbi wa shule hiyo Januari 31 mwaka huu ambapo walimu 15 na wanafunzi 55 walitunukiwa na mgeni rasmi Pascal Obed Busigo ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Msaidizi Sekondari Jiji la Mbeya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tehlah Foundation anatimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka jana katika mahafali ya kidato cha nne,endapo wanafunzi na walimu watafanikisha kupatikana matokeo mazuri na ndiyo dhamira yake kuona shule yake inafanya vizuri.
Shule hiyo yenye usajili namba S.3572 ambayo ina ushirikiano na Shirika la Gateway la Ujerumani ambapo  katika matokeo hayo shule imeshika nafasi ya kumi na tatu kiwilaya  kati ya shule 47,na hamsini na nane kimkoa kati ya shule 265,na  imekuwa shule ya 59 kikanda kati ya shule 464 katika matokeo hayo wanafunzi 127 waliofanya mtihani wote wamefaulu kuingia kidato cha tatu.

 Mkuu wa shule hiyo Eckson Mwakalikamo amesema mwaka uliyopita shule iliweka mikakati mbalimbali kama vile kuanzisha mitihani ya udahili kabla ya mwanafunzi kupokelewa shuleni ,nakufanya mitihani mara kwa mara,nakuanzisha masomo ya jioni ili walimu kumaliza mitaala mapema kabla ya mitihahani ya Taifa.

Kwa upande mgeni rasmi Pascal Busigo aliupongeza mpango wa shule hiyo wa kutoa tunu kwa walimu na wanafunzi kwani kufanya hivyo kutaifanya serikali kufikia mpango wake wa matokeo makubwa sasa maarufu kama BRN[Big Result Now].
Aidha Busigo aliwataka walimu,wazazi na wanafunzi kufanya kazi kwa ushirikiano kila mmoja kwa nafasi yake yaani walimu kufundisha vema,wazazi kulipa ada kwa wakati na wanafunzi kuzingatia masomo kufanya hivyo kutaleta tija huku nidhamu kwa walimu na wanafunzi ikipewa kipaumbele Mungu atabariki.

Alimaliza kwa kuwataka kuwa mabalozi wazuri wanafunzi wanaosoma shule hiyo kwani Taifa litajengwa na wasomi ambao watazingatia uzalendo badala ya kufanya vitendo viovu wawapo shuleni ambavyo vitapelekea kufanya vibaya katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne hivyo kupoteza mwelekeo wa maisha kwa ujumla.

Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Askofu Eliezery Kamwela aliwataka wanafunzi kumtegemea Mungu wakati wote wa masomo huku nidhamu ikipewa kipau mbele zaidi na kuwataka wazazi kusaidiana na walimu kuboresha ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.



Post a Comment

 
Top